Afrika

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Marufuku hii ya maji Johannesburg ni balaa!

Afrika Kusini: Wakazi Wa Johannesburg Washauri Wa Kuoga Kwa Dakika Marufuku hii ya maji Johannesburg ni balaa!

Mon, 18 Sep 2023 Chanzo: Bbc

Wasambazaji wa maji mjini Johannesburg, Afrika Kusini, wamewataka wakazi wa jiji hilo na vitongoji vyake kutumia maji kidogo huku ongezeko la uhaba wa maji ukitishia "kuanguka kwa mfumo".

Rand Water na Johannesburg Water siku ya Jumapili zilisema kuwa matumizi makubwa ya maji kwa wakazi "yanatatiza mfumo" na imesababisha viwango vya chini vya hifadhi ya maji.

Kampuni hizo zimewataka wakazi kuokoa maji kwa kupunguza kuoga hadi dakika mbili, kutumia maji chooni baada ya haja kubwa na kuosha magari wikendi pekee kwa kutumia ndoo.

Kampuni hizo pia zimewataka wakazi kuacha kujaza maji vidimbwa vya kuogelea hadi uhaba wa maji uishe, kuepuka kumwagilia bustani na nyasi kwa maji safi na kurekebisha au kutoa taarifa kuhusu uvujaji wa maji.

Johannesburg kwa sasa iko chini ya vikwazo vya kila mwaka vya maji, ambavyo mara nyingi hudumu wakati wa kiangazi cha Afrika Kusini kati ya Septemba na Machi.

Katika wiki za hivi karibuni, baadhi ya wakaazi wa jiji hilo na taasisi kama vile hospitali zimekosa maji, na kusababisha kutoridhika kwa umma.

Chanzo: Bbc