Afrika

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Martha Karua aahidi kumpigia debe Spika Muturi kuingia Ikulu 2022

4dd7c0e3d95dcdde Martha Karua aahidi kumpigia debe Spika Muturi kuingia Ikulu 2022

Sun, 8 Aug 2021 Chanzo: kiswahili.tuko.co.ke

Muturi alikutana na Karua katika kile amesema ni mpango wake wa kuleta viongozi pamoja kwa mjadala kuhusu umoja wa kitaifaKarua alikubali kuingia Boksi ya Muturi na ameahidi kuwa atamuunga mkono kwenye azma yake ya kuingia IkuluSpika alisema ifikapo 2022 ataondoka Jubilee na kuingia chama kingine ili kupanga karata zake za kuingia Ikulu kumrithi Rais UhuruKiongozi wa Chama cha Narc Kenya Martha Karua Jumamosi Agosti 7 alikutana na Spika wa Bunge Justin Muturi.

Muturi alisema kikao chao ni kwenye mpango wake wa kukutana na viongozi katoika kutafuta muungano kwenye safari yake ya kuingia Ikulu.

"Hii ni mojawapo wa vikao ambapo nafanya na viongozi katika kufanya mazungumzo kuhusu umoja wa kitaifa," Muturi alisema Jumamosi.

Alisema ataendeleza mazungumzo na viongozi wote katika azma yake ya kuingia ikulu kumrithi Rais Uhuru Kenyatta.

"Katika siku na wiki zijazo nitakuwa nawatafuta viongozi wote ili tuweze kujenga uhusianoi katika ajenda hii," aliongeza.

Read also

Magazeti Ijumaa Julai 6: DP Ruto Asema Atachomoka Kutoka Serikali Wakati Ukifika



“Endelea na mpango JB. Uko na uungwaji mkono katika safari hii. Nitatembea na wewe, nitakiutafutia uungwaji mkono,” Karua alisema.

"Nasubiri mikutano ambapo nitakuja na kuwaomba watu kukupigia kura ili uchukue kazi ya kuliongoza taifa," aliongeza kiongozi huyo wa NARC Kenya.

Muturi anamezea mate kiti cha urais na ameahidi kufanya kila liwezekanalo ili kuingia Ikulu.



Tangazo lake la kuingia Ikulu lilizua hisia kali za kisiasa haswa katika eneo la Mlima Kenya huku magavana kadhaa wakipinga kutawazwa kwake kama msemaji wa Mt Kenya.

Muturi alitawazwa katika enepo la Mukuru wa Nyagathanga na kuwakera baadhi ya viongozi waliokashifu hatua yake kuingia eneo la Mukuru wakisema hilo huwa eneo takatifu.

Gavana Mwangi wa Iria alisema alichofanya Muturi ilikuwa kuchafua eneo hilo takatifu na sarakasi zake za siasa.
Chanzo: kiswahili.tuko.co.ke