Afrika

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

TV

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Marekani yawekea vikwazo kundi la IS nchini Somalia

Marekani Yawekea Vikwazo Kundi La IS Nchini Somalia Marekani yawekea vikwazo kundi la IS nchini Somalia

Wed, 2 Nov 2022 Chanzo: Bbc

Marekani imeliwekea vikwazo kundi la Islamic State (IS) nchini Somalia na baadhi ya wanachama wake wanaodaiwa kusafirisha silaha kwa magendo Afrika Mashariki.

IS inaendesha shughuli zake kaskazini-mashariki mwa nchi ambako inalenga vikosi vya usalama na raia katika mashambulizi.

Licha ya kupata usaidizi wa kikanda na kimataifa, Somalia inaendelea kukabiliwa na ghasia mbaya za wanamgambo. IS Somalia imekuwa ikifanya kazi katika taifa hilo la Pembe ya Afrika tangu 2015.

Watu waliowekewa vikwazo wanatuhumiwa kutoa msaada kwa kitengo cha kijasusi cha kundi hilo, kusafirisha silaha kwa njia ya magendo kote Afrika Mashariki na kuratibu mashambulizi ya hali ya juu.

Baadhi walikuwa wanachama wa zamani wa kundi la al-Shabab. Mnamo Oktoba, Marekani iliorodhesha wanachama kadhaa wa al-Shabab pia wanaosemekana kuwa wanasafirisha silaha kati ya Somalia na Yemen ambapo al-Qaeda na Islamic State wamejikita.

Mashambulizi makali ya makundi ya wanamgambo wa Somalia yamegharimu maisha ya watu wengi na kuzua hofu kubwa.

Somalia inategemea sana usaidizi wa kimataifa ili kuvuruga silaha haramu na mitandao ya ufadhili ya shughuli za al-Shabab na Islamic State.

Chanzo: Bbc