Afrika

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Marekani yawaka Sudan kumuachilia muuaji wa mwanadiplomasia

Mjnhkmjnjy Marekani yawaka Sudan kumuachilia muuaji wa mwanadiplomasia

Thu, 2 Feb 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Marekani inasema inahofu kubwa kuhusu kuachiliwa kwa mwanaume wa Sudan anayekabiliwa na hukumu ya kifo kuhusiana na mauaji ya mwanadiplomasia wa Marekani miaka 15 iliyopita.

Maafisa nchini Sudan Jumatatu walimuachilia huru Abdel -Rauf Abu Zaid, ambaye alipatikana na hatia ya mauaji ya John Granville na dereva wake Msudan Abdel Rahman Abbas.

Waliuawa kwa risasi na wanamgambo wa Kiislam katika siku ya Mwaka mpya 2008.

Wizara ya mambo ya nje ya Marekani ilikanusha kwamba kuachiliwa kwao ilikuwa ni sehemu ya makubaliano ya nchi mbili.

Ilisema inasumbuliwa na ulosefu wa uwazi katika mchakato wa sheria.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live