Afrika

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Marekani yatoa tamko maandamano Kenya

MAANDAMANO YENYE GHASIA Marekani yatoa tamko maandamano Kenya

Thu, 30 Mar 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Marekani imetoa wito kwa pande zote za kisiasa nchini Kenya kuachana na ghasia na vikosi vya usalama kuzingatia utu wanapokabiliana na waandamanaji.

Naibu msemaji wa Wizara ya Mambo ya Nje Vedant Patel, amesema Marekani imesikitishwa na vifo vilivyotokea pamoja na uharibifu wa mali katika maandamano akibainisha kuwa maandamano ya amani ni haki ya kidemokrasia.

"Tunawahimiza viongozi wa kisiasa, waandamanaji na vyama vyote kujiepusha na ghasia na matamshi ambayo yanaweza kuchochea ghasia,"

Kiongozi wa upinzani nchini Kenya Raila Odinga ametangaza kufanyika kwa maandamano kila Jumatatu na Alhamisi kupinga kupanda kwa gharama za maisha pamoja na uchaguzi wa haki ambapo maandamano hayo yamezusha vurugu na kusabaisha vifo vya watu wawili na uharibifu wa mali.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live
Related Articles: