Afrika

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

TV

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Marekani yatoa tahadhari ya usalama kwa raia wake waishio Kenya

Marekani Yatoa Tahadhari Ya Usalama Kwa Raia Wake Waishio Kenya Marekani yatoa tahadhari ya usalama kwa raia wake waishio Kenya

Wed, 26 Jul 2023 Chanzo: Bbc

Ubalozi wa Marekani Jumanne, Julai 25 ulitoa ushauri wa usalama kwa raia wake kabla ya matukio ya kuwakumbuka waathiriwa wa vurugu za maandamano yaliyoandaliwa Muungano wa Azimio la Umoja.

Katika taarifa yake, ubalozi huo umeonya kuwa matukio hayo yanayotarajiwa kufanyika kote nchini humo yanaweza kugeuka kuwa ghasia licha ya hakikisho kutoka kwa upinzani kwamba yatakuwa ya amani.

Kulingana na ushauri, usumbufu wa msongamano wa magari unaweza kutokea. Kwa hivyo ubalozi umewashauri raia wa Marekani kuepuka maeneo ambayo matukio ya kumbukumbu yatakayoambatana na matembezi yatafanyika, kufuatilia vyombo vya habari vya ndani kwa ajili ya kupata taarifa, na kuepuka mikusanyiko ya watu.

Hatua za kuchukua ni pamoja na kufahamu mazingira yako, kukagua mipango yako ya usalama wa kibinafsi na kubeba Kitambulisho sahihi.

"Kuwa na mipango ya uokoaji ambayo haitegemei serikali ya Marekani," ilisema taarifa hiyo.

Muungano wa Azimio unaoongozwa na aliyekuwa Waziri Mkuu Raila Odinga unatarajiwa kufanya kumbukumbu kote nchini humo kwa heshima ya Wakenya waliopoteza maisha wakati wa maandamano ya kuipinga serikali yaliyoandaliwa wiki zilizopita.

Chanzo: Bbc