Afrika

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Marekani yatangaza vikwazo kwa wahujumu Demokrasia Nigeria

Antony Blinken Waziri wa mambo ya nje wa Marekani Antony Blinken

Thu, 26 Jan 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Waziri wa mambo ya nje wa Marekani Antony Blinken ametangaza vikwazo vya viza kwa baadhi ya Wanigeria wanaotuhumiwa kuhujumu Demokrasia na kubainisha kuwa watu waliowekewa vikwazo hivyo hawatastahili kupata visa vya Marekani.

“Tumejitolea kuunga mkono na kuendeleza demokrasia nchini Nigeria na duniani kote. Leo, ninatangaza vikwazo vya visa kwa watu mahususi nchini Nigeria kwa kuhujumu mchakato wa kidemokrasia katika uchaguzi wa hivi majuzi wa Nigeria.

“Chini ya Kifungu cha 212(a)(3)C) cha Sheria ya Uhamiaji na Uraia, watu hawa hawastahili viza ya kuingia Marekani chini ya sera ya kuzuia visa vya wale wanaoaminika kuwajibika, au kushiriki katika kuhujumu demokrasia nchini Nigeria.

"Wanafamilia wa watu kama hao wanaweza pia kuwa kwenye vizuizi hivi.” Blinken alisema, akifafanua kuwa kizuizi hicho hakilengi. Watu wa Nigeria au serikali.

Hatua hii ya Marekani inakuja Takriban wiki mbili baada ya serikali ya Uingereza kuapa kuweka marufuku ya viza kwa wanasiasa wa Nigeria wanaohusika na ghasia na wizi wa kura.

Aidha Kamishna Mkuu wa Uingereza nchini Nigeria, Catriona Liang, wiki mbili zilizopita, alisema kwamba mtu yeyote ambaye anachochea ghasia au vurugu ili kudhoofisha mchakato wa uchaguzi wa 2023 atazuiwa kuzuru Uingereza.

Liang alizungumza hayo alipokuwa akijibu malalamiko ya Mwenyekiti wa Taifa wa Chama cha Labour (LP), Bw. Julius Abure, kuhusu mauaji ya wagombea na viongozi wa chama chake katika maeneo mbalimbali nchini.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live