Afrika

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Marekani yataifisha jumba la kifahari la aliyekuwa Rais wa Gambia – Millardayo.com

C7856d42 C874 4b34 Bede 504c1730aca1 Mansion Jumba la Yahya Jammeh

Sat, 18 Jul 2020 Chanzo: millardayo.com

Wizara ya sheria Marekani imesema kwamba aliyekuwa Rais wa Gambia Yahya Jammeh alitumia pesa alizopata kwa njia ya ufisadi na ubadhirifu wa fedha za umma kununua jumba la kifahari huko Washington alipokuwa madarakani.

Kulingana na nyaraka zilizowasilishwa kama sehemu ya juhudi za kutwaa jengo hilo katika Mji Mkuu wa Marekani, Jammeh alinunua jumba hilo lenye thamani ya Dola Milioni 3.5 za Marekani sawa na  na zaidi ya Bilioni saba za Kitanzania miaka 10 iliyopita.

Inasemekana kwamba alinunua jumba hilo kupitia Mke wake Zineb Jammeh.

Jammeh alitoroka Nchi baada ya kushindwa kwenye uchaguzi wa 2017 na sasa hivi anaishi nchini Equatorial Guinea.

Chanzo: millardayo.com