Afrika

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Marekani yasaidia vifaa kujikinga na corona

3eedefeb83dfaf752f83c453f5585e8b Marekani yasaidia vifaa kujikinga na corona

Tue, 18 Aug 2020 Chanzo: habarileo.co.tz

MAREKANI imetoa vifaa tiba vyenye thamani ya faranga milioni 31 kwa ajili ya kusaidia Rwanda kupambana na ugonjwa wa homa kali ya mapafu (covid-19) unaosababishwa na virusi vya corona.

Msaada huo uliokabidhiwa juzi na Balozi wa Marekani nchini humo, Peter Vrooman, ni barakoa kwa ajili ya upasuaji, vifaa vya kutumia wakati wa kujifungua na glovu.

Vifaa vingine ni vya kusaidia wagonjwa wa covid-19 kupumua, vitakasa mikono, sabuni za kunawa mikono na vitanda vya kulaza wagonjwa.

Taarifa iliyotolewa na ubalozi wa Marekani ilieleza kuwa, vifaa hivyo vitasambazwa kwa wafanyakazi wa afya wanaotoa huduma kwa wagonjwa hao wakiwemo madaktari, wauguzi na wengine katika vituo vya afya 349 na hospitali 25 za wilaya, majimbo na rufaa.

Vifaa hivyo ni sehemu ya faranga zaidi ya bilioni 11 zilizotolewa na nchi hiyo kwa Rwanda kwa ajili ya kupambana na ugonjwa huo, pamoja na ujenzi wa maeneo ya kunawa mikono katika wilaya zote na kusaidia mawasiliano kwa umma juu ya namna ya kupambana na covid-19.

Marekani imeisaidia Rwanda zaidi ya dola za Marekani bilioni 1.5 zilizowekezwa katika afya ya umma katika miaka 20 iliyopita nchini humo.

Chanzo: habarileo.co.tz