Afrika

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Marekani yamwekea vikwazo Rais Mnangagwa

Emmerson Mnangagwa Zimbabwe Election 860x573 Marekani yamwekea vikwazo Rais Mnangagwa

Tue, 5 Mar 2024 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Marekani imewawekea vikwazo watu tisa 9 nchini Zimbabwe akiwemo Rais wa nchi hiyo, Emmerson Mnangagwa, mke wake, Auxillia Mnangagwa, Makamu wa Rais, Constantino Chiwenga, Waziri wa Ulinzi, Mkuu wa Upelelezi wa Zimbabwe na Patrick Chinamasa Mweka Hazina wa chama cha kisiasa cha Zanu PF.

Pia Marekani imeyawekea vikwazo Makampuni matatu ya kibiashara ya Zimbabwe. Marekani inawashutumu viongozi hao kuhusika katika ukiukwaji wa haki za binadamu, rushwa, utekaji wa watu na unyanyasaji uliopitiliza.

Vikwazo hivyo ni pamoja na kukamatwa kwa nyumba zao zilizopo kwenye ardhi ya Marekani na kutoruhusiwa kuingia nchini humo. Hadi kufikia sasa uongozi nchini Zimbabwe haujatangaza kitu chochote kuhusiana na hatua hiyo.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live