Afrika

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Marekani yamuwekea vikwazo mtoto wa rais wa Zimbabwe

Marekani Yamuwekea Vikwazo Mtoto Wa Rais Wa Zimbabwe Marekani yamuwekea vikwazo mtoto wa rais wa Zimbabwe

Tue, 13 Dec 2022 Chanzo: Bbc

Marekani imewawekea vikwazo vya kifedha raia wanne wa Zimbabwe akiwemo mtoto wa rais Emmerson Mnangagwa.

Inamshutumu Emmerson Mnangagwa Junior kwa kuhusishwa na mfanyabiashara, Kudakwashe Tagwirei, ambaye tayari yuko chini ya vikwazo vya Marekani kwa madai ya ufisadi.

Idara ya Hazina inasema katika miaka mitano iliyopita, Bw Tagwirei ametumia mseto wa biashara zisizoeleweka na uhusiano wake unaoendelea na rais kukuza biashara yake kwa kiasi kikubwa na kupata mamilioni ya dola.

Rais Mnangagwa tayari yuko chini ya vikwazo vya Marekani.

Katika taarifa yake, Idara ya Hazina iliitaka serikali ya Zimbabwe kushughulikia kile ilichokiita chanzo cha maovu mengi nchini humo, ikiwa ni pamoja na wasomi wafisadi kutumia vibaya taasisi kwa manufaa yao binafsi.

Chanzo: Bbc