Afrika

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Marekani yalaumiwa kukwamisha mchakato wa amani DRC

Mlinda Amani Auwawa, Na Mwengine Kujeruhiwa DRC Marekani yalaumiwa kukwamisha mchakato wa amani DRC

Tue, 28 Feb 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Serikali ya Rwanda imesema kwamba matamshi ya Marekani kuhusu mzozo wa mashariki mwa Kongo na kuishutumu Rwanda kuwa inawaunga mkono waasi la M23 yanaweza kudhoofisha juhudi za kikanda za kuutafutia ufumbuzi mgogoro wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo.

Viongozi wa Afrika waliokutana nchini Ethiopia Februari 17 waliwapa waasi wa M23 muda wa hadi tarehe 30 Machi kuondoka katika maeneo yote wanayoyakaliwa kwa mabavu ya mashariki mwa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo.

Wizara ya Mambo ya Nje ya Marekani katika taarifa yake wiki iliyopita iliitaka Rwanda "ikomeshe uungaji mkono wake kwa waasi wa M23 na kuruhusu kufanikiwa mchakato wa amani unaondeshwa na kusimamiwa na Jumuiya ya Afrika Mashariki.

Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo imekuwa ikiishutumu Rwanda kwa kuwaunga mkono waasi wa M23, madai ambayo Rwanda inayakanusha mara kwa mara.

Kwa upande wake Kigali inawatuhumu wanajeshi wa Kongo kuwa wanashirikiana na waasi wa Rwanda wa chama cha Democratic Forces for the Liberation of Rwanda (FDLR).

Serikali ya Kigali pia imeilalamikia jamii ya kimataifa kwa kile ilichosena ni "kushindwa mara kwa mara" kuilaani Kinshasa kwa ilichodai ni "kuwapa hifadhi" waasi wa Rwanda wa FDLR nchini Kongo.

Sehemu moja ya taarifa ya serikali ya Rwanda imesema: "Hatuwezi kukubali kudharauliwa na kupuuzwa wasiwasi tulio nao kuhusu usalama wa nchi yetu."

Kuibuka tena kwa M23 kumeongeza mvutano kati ya nchi mbili jirani za Rwanda na Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo. Tangu mwaka jana, waasi wa M23 wameteka miji muhimu katika jimbo la Kivu Kaskazini.

Mji wa hivi karibuni zaidi uliotekwa na waasi wa M23 ni ule wa kimkakati wa Rubaya wenye utajiri mkubwa wa madini. Ulitekwa na waasi hao siku ya Jumapili ya juzi.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live