Afrika

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Marekani yakana kuhusika na kuporomoka kwa uchumi Zimbabwe

Sanctions Marekani yakana kuhusika na kuporomoka kwa uchumi Zimbabwe

Mon, 25 Oct 2021 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Marekani imetetea hatua yake ya kuweka vizuizi vya kiuchumi nchini Zimbabwe kwa zaidi ya miongo miwili kwa kusema kuwa ilifanya hivyo ili kudhibiti vitendo visivyo vya kidemokrasia, ufisadi na uvunjifu wa haki za bianadamu nchini humo.

Kauli hii imetolewa na msemaji wa Idara ya majimbo nchini Marekani Ned Prince, mara baada mwandishi maalum wa Umoja wa Mataifa anayeshughulikia masuala ya utambuzi wa athari za ukiukwaji wa haki za binadamu kuwasili nchini Zimbabwe kwajili ya kufuatilia mwenendo wa demokrasia nchini humo.

Mwandishi huyo kutoka Belarusi Alena Douhan anatarajia kukutana na Rais Emmerson Mnagangwa wa Zimbabwe jumatatu ya Oktoba 25, 2021 kwa ajili ya kuanza ziara yake ya siku 10 ambayo itahusisha mikutano ya pamoja na viongozi wa ngazi za juu Serikalini.

Aidha Ned Prince amesisitiza kuwa Marekani haihusiki na kuporomoka kwa uchumi wa Zimbabwe kama ambavyo indaiwa kufuatia kuwekwa kwa vizuizi vikali nchini humo.

"Vizuizi tulivyoweka nchini humo vinawalenga wale wote wanaovunja misingi ya haki za binadamu na wale wote ambao wanakiuka demokrasia au kuhusika na vitendo vya rushwa na ufisadi"

"Napenda kuweka wazi hili kua vizuizi hivi havikulenga kugusa maisha ya wanachi wa kawaida nchini Zimbabwe, na kuporomoka kwa uchumi wa taifa hilo kumesababishwa viongozi waliolewa madaraka na sio sisi Marekani" amesema Prince.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live