Afrika

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Marekani yaiunga mkono Morocco kutawala Sahara

Wendy Sherman Naibu Waziri wa Mambo ya Nje wa Marekani Wendy Sherman

Wed, 9 Mar 2022 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Marekani siku ya Jumanne ilisisitiza kuunga mkono mpango wa Morocco wa kujitawala katika ukanda wa Sahara Magharibi ili kusuluhisha mzozo wa miongo kadhaa wa ufalme huo na vuguvugu la kudai uhuru la Polisario.

"Tunaendelea kuutazama mpango wa kujitawala wa Morocco kwa uzito na ni mpango wa kuaminika ," Naibu Waziri wa Mambo ya Nje wa Marekani Wendy Sherman alisema wakati wa ziara yake kwa mshirika wa Marekani.

Sherman alionyesha kumuunga mkono Staffan de Mistura, mjumbe wa Umoja wa Mataifa katika Ukanda huo, ambaye anafanya kazi ya kufufua mchakato wa amani ambao umekwama tangu 2019.

"Tunafanya hivyo kwa nia iliyo wazi kutafuta azimio ambalo litapelekea matokeo ya kudumu na yenye heshima kwa pande zote," Sherman aliwaambia waandishi wa habari baada ya kukutana na mwanadiplomasia mkuu wa Morocco Nasser Bourita.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live