Afrika

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Marekani yaiondoa Nigeria kwenye orodha ya nchi zinazokiuka dini

AP 21083461864124 Marekani yaiondoa Nigeria katika orodha ya wanaokiuka dini

Thu, 18 Nov 2021 Chanzo: BBC

Marekani imeiondoa Nigeria katika orodha ya wanaokiuka dini, kabla ya ziara ya Waziri wa Mambo ya Nje Antony Blinken nchini humo.

Serikali ya Marekani mwaka jana iliiweka Nigeria katika orodha yake maalum ya waangalizi wa mataifa ambayo yaliendekeza ukiukwaji mkubwa wa uhuru wa kidini.

Nigeria haimo katika orodha ya 2021 ambayo ina Myanmar, China, Eritrea, Iran, Korea Kaskazini, Pakistan, Russia, Saudi Arabia, Tajikistan na Turkmenistan.

Algeria, Comoro, Cuba, na Nicaragua pia zimo kwenye orodha maalum ya serikali ambazo zimekiuka uhuru wa kidini, kulingana na idara ya masuala ya kigeni ya Marekani.

Hata hivyo, makundi ya kijihadi ya Boko Haram na Iswap linaloendesha shughuli zake kaskazini-mashariki mwa Nigeria, bado yanatia wasiwasi.

Bw Blinken anazuru Nigeria siku ya Alhamisi katika awamu ya pili ya safari yake ya mataifa matatu ambayo ni pamoja na Kenya na Senegal.

Anatarajiwa kukutana na Rais wa Nigeria Muhamadu Buhari kujadili jinsi nchi zote mbili zinaweza kushirikiana zaidi katika afya ya kimataifa, usalama, kupanua upatikanaji wa nishati na ukuaji wa uchumi.

Nigeria inapambana na vitisho vingi vya usalama, vikiwemo uasi wa muda mrefu wa Boko Haram, mapigano baina ya jamii na hivi karibuni, wimbi la utekaji nyara mkubwa shuleni unaofanywa na magenge yenye silaha.

Chanzo: BBC