Afrika

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Marekani yahofia hali ya afya rais aliyeondolewa madarakani Niger

Marekani Yahofia Hali Ya Afya Rais Aliyeondolewa Madarakani Niger Marekani yahofia hali ya afya rais aliyeondolewa madarakani Niger

Thu, 10 Aug 2023 Chanzo: Bbc

Marekani na Umoja wa Mataifa zatilia shaka hali ya kiafya na kiusalama ya Rais wa Niger Mohamed Bazoum, ambaye amekuwa akizuiliwa kwa zaidi ya wiki.

"Tuna wasiwasi mkubwa kuhusu afya yake na usalama wake binafsi na usalama wa kibinafsi wa familia yake," msemaji wa idara ya serikali ya Marekani alisema.

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Antonio Guterres pia alisema ana wasiwasi, ikiwa ni pamoja na kuhusu "hali mbaya ya maisha" ambayo familia hiyo ilikuwa nayo.

Bw Bazoum aliondolewa madarakani tarehe 26 Julai.

apo awali chama cha Bw Bazoum kilisema kuwa yeye na familia yake walikuwa wakizuiliwa katikamazingira ya "katili" na "isiyo ya kibinadamu," Reuters iliripoti.

Tangu wakati huo, utawala wa kijeshi umekuwa ukiongoza Niger huku Bw Bazoum akizuiliwa katika ikulu ya rais. Jeshi halijatoa kauli yoyote kuhusu hali ya kiongozi huyo aliyeondolewa madarakani.

Siku ya Jumanne Waziri wa Mambo ya Nje wa Marekani Antony Blinken alimpigia simu Bw Bazoum akimhakikishia uungwaji mkono wa Marekani, Washington ilisema.

Msemaji wa Wizara ya Mambo ya Nje ya Marekani Matthew Miller aliongeza: "Kadiri muda unavyosonga, huku akiendelea kushikiliwa, ni hali ambayo inazidi kututia wasiwasi."

Chama cha kisiasa cha Bw Bazoum, PNDS-Tarayya, kilidai katika taarifa kwamba Bw Bazoum na familia yake hawakuwa na maji ya bomba, umeme, bidhaa safi wala madaktari.

Kauli hiyo iliangazia maoni ya awali yaliyotolewa na waziri mkuu mteule wa Niger Ouhoumoudou Mahamadou, ambaye amesema Bw Bazoum alikuwa akishikiliwa na mkewe na mwanawe bila umeme wala maji.

Chanzo: Bbc
Related Articles: