Afrika

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Marekani yahimiza majadiliano mzozo wa DRC

Kifo Cha Mpinzani Wa DRC Cherubin Okende Ni Kitendo Cha Kujiua Mwendesha Mashtaka Marekani yahimiza majadiliano mzozo wa DRC

Mon, 22 Apr 2024 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Marekani kupitia maafisa wake wawili walioitembelea DRC mwishoni mwa juma lililopita inasema inaamini kuwa mgogoro wa kivita unaoshuhudiwa mashariki mwa nchi hiyo unapaswa kutatuliwa kwa njia ya mazungumzo.

Kwa mujibu wa wajumbe hao wawili wa Marekani ambao ni Enrique Roig, naibu katibu msaidizi wa serikali katika ofisi kuu inayojihusisha na demokrasia, utawala na amani katika Idara inayosimamia majimbo, na Mark Billera, naibu msimamizi katika ofisi kuu na yenyewe ikiwa yenye kusimamia demokrasia ya USAID, ni kuwa matumizi ya silaha huko mashariki mwa Jamhuri ya kidemokrasia ya Congo inayoshuhudiwa haiwezi kusuluhisha mgogoro kati ya serikali ya Kinshasa na waasi wa M23.

Maafisa Hao wawili wa Marekani walithibitisha hayo siku ya Jumamosi ya Aprili 20 mjini Kinshasa, mwishoni mwa ziara ya wiki moja ambapo walitembelea mamia kwa maelfu ya wakimbizi kwenye makambi nchini DRC.

Enrique Roig aliwaambia waandishi wa habari mjini Kinshasa kwamba wanafanya kazi na maafisa Wa Congo lakini pia na washirika wa kikanda kutafuta suluhu ya matatizo ya Mashariki mwa nchi hiyo, na kwamba anafahamu jukumu lililotekelezwa na M23, chini ya vikwazo vya kimataifa kundi ambalo amekiri linaungwa mkono na Rwanda, huku akithibitisha kuwa wamihimiza nchi ya Rwanda kukubali kuwaondoa mara moja wanajeshi wake nchini DRC na kumwajibisha mtu yeyote anayetuhumiwa kufanya ukiukaji wa haki za binadamu.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live