Afrika

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Marekani waiomba DRC iwalinde walinda amani nchini humo

Images (33).jpeg Marekani waiomba DRC iwalinde walinda amani nchini humo

Sat, 30 Jul 2022 Chanzo: VOA

Marekani imeiomba serikali ya DRC kuwalinda walinda amani wa Umoja wa Mataifa na majengo yao kufuatia maandamano yanayoendelea nchini humo.

Maandamano ya kuipinga Tume ya UN nchini humo, inayojulikana kama MONUSCO, yamezuka tangu Jumatatu na kusababisha vifo vya watu 19 ikiwemo walinda amani wa UN watatu.

Msemaji wa Wizara ya Mambo ya Nje wa Marekani Ned Price amesema, Marekani inatoa wito kwa taifa na mamlaka za ndani za DRC kuhakikisha ulinzi wa MONUSCO, maeneo yao na wanajeshi na waandamanaji kujieleza kwa njia ya amani.

Marekani imesema mashambulizi dhidi ya maafisa wa UN na maeneo yao ni kinyume cha sheria za kimataifa na inashukuru nia ya dhati ya DRC kuchunguza vitendo hivyo.

Chanzo: VOA