Afrika

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Marekani kuwawekea vikwazo wahusika wa vita DRC

Waasi 17 Drc Marekani kuwawekea vikwazo wahusika wa vita DRC

Mon, 11 Dec 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Marekani imetangaza vikwazo dhidi ya watu kadhaa nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC). Miongoni mwao, William Yakutumba, Willy Ngoma na Michel Rukunda, ambao kwa mujibu wa Washington, "wanachangia kwa kuhatarishwa kwa usalama kwa sasa" nchini.

Jumla ya watu watano wanalengwa na vikwazo hivi kwa jukumu lao katika mzozo unaosambaratisha Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo. Anayeongoza ni William Yakutumba. Kulingana na Washington, kiongozi wa wanamgambo wa Mai-Mai Yakutumba, wanaoendesha uhalifu wao hasa katika mkoa wa Kivu Kusini, anahusika katika vitendo vya ubakaji.

Kuajiri watoto

Akiwa analengwa pia na vikwazo hivyo, msemaji wa M23 Willy Ngoma, ambaye kundi lake linasemekana kuhusika na ukiukaji wa haki za binadamu. Pia katika orodha ya Marekani yumo Michel Rukunda, kiongozi wa kundi la Twirwaneho anayeshutumiwa kwa kuwaandikisha watoto kushiriki katika mapigano au kufanya kazi katika kambi za kijeshi. Mali zazuiwa

Hatimaye, watu wawili wanaohusishwa na kundi la Islamic State kwa Afrika ya Kati pia wameguswa na vikwazo hivi. Kwa hivyo, mali zote zinazowezekana za watu hawa nchini Marekani zitazuiwa, na makampuni na taasisi haziruhusiwi kudumisha mawasiliano yoyote na watu hawa. Kwa mujibu wa Washington, ni swali la "kubainisha kujitolea kwao kutumia njia zote za kidiplomasia na kisheria kuwatenga wale wanaodhoofisha utulivu na usalama" nchini DRC.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live