Afrika

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Marekani imeirejesha Mauritania kwenye mpango wa AGOA

Biden Aionya Iran Katika Ujumbe Adimu Wa Moja Kwa Moja Marekani imeirejesha Mauritania kwenye mpango wa AGOA

Wed, 1 Nov 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Marekani imesema itarejesha nchi ya Mauritania kwenye mpango wa kibiashara kati yake na bara Afrika (Agoa) kufuatia tathmini ya ustahiki.

Kwa mujibu wa Washington, mpango huo unatarajiwa kufanyika mwezi Januari mwaka ujao baada ya nchi hiyo ya kaskazini-magharibi mwa Afrika kufanya kile ambacho kimetajwa kuwa maendeleo makubwa na yanayoweza kutathiminiwa kuhusu haki za wafanyakazi.

Washington ilisitisha manufaa ya kibiashara mwaka wa 2019 kufuatia wasiwasi juu ya ukiukaji wa haki za wafanyikazi nchini Mauritania.

Kurejeshwa kwa Mauritania kunafuatia tangazo la Rais wa Marekani Joe Biden siku ya Jumanne la kusitisha uanachama wa Gabon, Niger, Uganda na Jamhuri ya Afrika ya Kati (CAR) kutoka kwenye mpango huo.

Marekani ilisema ilichukua hatua hiyo dhidi ya mataifa ya Gabon na Niger kwa sababu ya mabadiliko ya serikali kinyume na katiba baada ya mapinduzi, wakati uanachama wa Uganda na Jamhuri ya Afrika ya Kati ukisitishwa kwa madai ya ukiukaji wa haki za binadamu unaofanywa na serikali za mataifa hayo.

Burkina Faso, Mali na Guinea zote zimeondolewa kutoka mpango wa Agoa baada ya mapinduzi ya kijeshi katika nchi hizo.

Uchumi wa Mauritania unatawaliwa na viwanda vya uchimbaji, hasa mafuta na madini, ambavyo vinachangia zaidi ya robo tatu ya mauzo ya nje. Uvuvi, mifugo na kilimo cha mimea pia huchangia asilimia kubwa ya mapato ya serikali.

Mpango wa biashara wa Marekani na Afrika, ulioanzishwa mwaka wa 2000, unazipa nchi za Afrika Kusini mwa Jangwa la Sahara uwezo wa kusafirisha bidhaa zake hadi nchini Marekani bila kutozwa ushuru kwa zaidi ya bidhaa 1,800.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live