Afrika

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Marekani, Saudi Arabia washtumu kurejea kwa ghasia Sudan

Marekani, Saudi Arabia Washtumu Kurejea Kwa Ghasia Sudan Marekani, Saudi Arabia washtumu kurejea kwa ghasia Sudan

Mon, 12 Jun 2023 Chanzo: Voa

Marekani na Saudi Arabia zimeshtumu kuanzishwa tena kwa ghasia katika mji mkuu wa Sudan, Khartoum, ambapo wakaazi wameripoti mashambulizi ya anga na kukabiliana kwa silaha.

Katika taarifa ya pamoja nchi hizo mbili zilibainisha kuwa jeshi la Sudan na Vikosi vya Rapid Support Forces vilidhibiti vikosi vyao wakati wa usitishaji mapigano wa masaa 24, na inasikitisha sana kwamba mapigano yalianza tena.

Kikundi cha ujirani kinachounga mkono demokrasia kimesema makombora yametua katika makazi ya watu kusini mwa mji mkuu kufuatia kumalizika kwa muda wa usitishaji mapigano.

Mkazi mmoja aliyeamshwa na sauti ya mapigano, alisema utulivu wa siku moja Jumamosi ni sawa na ndoto ambayo sasa imetoweka.

Chanzo: Voa