Afrika

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

TV

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Marekani, Kenya wasaini hati ya makubaliano

Kijeshi Marekani Kenya (600 X 315) Marekani, Kenya wasaini hati ya makubaliano

Tue, 26 Sep 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Marekani na Kenya wamesaini makubaliano ya ulinzi yatakayosaidia taifa hilo la Afrika Mashariki kupata vifaa na msaada kwa wanajeshi wakati taifa hilo likijiandaa kuongoza kikosi cha kimataifa cha amani nchini Haiti, ambacho kitasaidia nchi hiyo kuimarisha usalama.

DW Swahili imeripoti kuwa kwa sasa Haiti inapambana na machafuko yanaoyasababishwa na makundi ya uhalifu na hasa katika mji mkuu Port-au-Prince. Waziri wa Ulinzi wa Marekani Lloyd Austin na mwenzake wa Kenya, Aden Duale, wamesaini makubaliano hayo katika mkutano uliofanyika jijini Nairobi, Kenya.

Imeelezwa kuwa makubaliano hayo yanajikita katika uhusiano wa kiulinzi kwa miaka mitano ijayo, wakati taifa hilo likiongeza harakati zake dhidi ya kundi la wanamgambo wa Al-Shabaab.

Austin ameishukuru Kenya kwa kujitolea kuongoza ujumbe wa amani nchini Haiti na kusema kwa mara nyingine kwamba Serikali ya Marekani itashirikiana na Bunge ili kupata dola milioni 100 za ufadhili ilizoahidi.

Moja ya makundi yanayotishia usalama nchini humo na hasa katika Mji Mkuu wa Port-au-Prince, ni lile linaloongozwa na aliyewahi kuwa ofisa wa polisi Jimmy Charizier maarufu ‘Barbecue,’ huku yakishinikiza serikali ya Haiti ijiuzulu.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live