Afrika

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

TV

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Marais wa Ufaransa, Marekani kukutana mazungumo ya kibiashara na usalama

Marais Wa Ufaransa, Marekani Kukutana Mazungumo Ya Kibiashara Na Usalama Marais wa Ufaransa, Marekani kukutana mazungumo ya kibiashara na usalama

Wed, 30 Nov 2022 Chanzo: Bbc

Rais wa Ufaransa Emmanuel Macro anatarajiwa kukutana na mwenzake wa Marekani Joe Biden hapa Washington DC kujadiliana maswala kadhaa yakiwemo ya kusawazisha sera za Marekani na Ufaransa kuhusu uvamizi wa Russia nchini Ukraine, na namna ya kurahihisha biashara.

Macron anakuwa rais wa kwanza kupata mwaliko wa kitaifa mara mbili, mara ya kwanza ikiwa mwaka 2018 wakati wa utawala wa Donald Trump, amapo alitolewa heshima kwa kufyatuliwa mizinga 21.

Ataandamana na mawaziri na wanadiplomasia kadhaa, pamoja na viongozi wa kibiashara.

Maafisa wa serikali ya Ufaransa wamesema kwamba kuna maswala muhimu ambayo Marekani inaweza kushirikiana na Ufaransa.

Ushirikiano kati ya Marekani na Ufaransa umepungua kwa mwaka mmoja sasa, tangu Marekani ilipopata mkataba wa gharama kubwa, wa uuzaji wa nyambizi kwa Australia na kuanzisha ushirikiano na Uingereza katika bahari ya Pacific.

Chanzo: Bbc