Afrika

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Marais kukutana Msumbiji kujadili mashambulizi

4b642d71405e8c2f063fa903f1618c16.jpeg Marais kukutana Msumbiji kujadili mashambulizi

Fri, 9 Apr 2021 Chanzo: www.habarileo.co.tz

VIONGOZI sita wa Afrika wanatarajia kukutana jijini Maputo, Msumbiji katika mkutano wa dharura utakaoangazia mashambulizi yanayotokea Kusini mwa Afrika: Imeripoti tovuti ya Serikali ya Zimbabwe.

Jumuiya ya Maendeleo Kusini mwa Afrika (SADC) imeitisha mkutano huo.

Ukiondoa Msumbiji ambayo ndiye mwenyeji wa mkutano, mataifa mengine yatakayokuwepo katika mkutano huo ni Afrika Kusini, Botswana, Zimbabwe, Malawi na Tanzania.

Rais wa Zimbabwe Emmerson Mnagngawa tayari ameondoka katika kikao hicho.

Awali, Rais wa Msumbiji Filipe Nyusi alisema ataitisha mkutano wa Baraza la Ulinzi na Usalama, lakini hakuweka wazi ni lini mkutano huo utafanyika.

Wanamgambo wa Kiislamu (IS) walivamia mji wa Palma uliopo Kaskazini mwa Jimbo la Cabo Delgado Machi 24, na kuua watu kadhaa na mamia kulazimika kukimbia makazi yao huku wengine wakikimbilia Tanzania.

Kundi la IS lilidai kuhusika na shambulio hilo likilenga eneo hilo tangu Oktoba mwaka 2017.

Hivi karibuni shambulio lililazimisha kampuni kubwa ya nishati ya Ufaransa kusitisha mipango yake ya uzalishaji wa gesi asilia katika eneo la Afungi Peninsula.

Chanzo: www.habarileo.co.tz