Afrika

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Marafiki watoa heshima zao kwa wanandoa waliouawa Uganda

Marafiki Watoa Heshima Zao Kwa Wanandoa Waliouawa Uganda Marafiki watoa heshima zao kwa wanandoa waliouawa Uganda

Thu, 19 Oct 2023 Chanzo: Bbc

Marafiki wametoa heshima kwa wanandoa waliouawa kwenye fungate pamoja na kiongozi wao katika Mbuga ya Kitaifa ya Queen Elizabeth nchini Uganda.

Wanandoa hao wametajwa kama David na Celia Barlow, kutoka Hampstead Norreys, karibu na Newbury huko Berkshire.

Klabu ya kriketi ya kijiji hicho ilisema "itawakosa sana" huku baraza la parokia likimwita Bw Barlow "nguzo ya jamii".

Polisi wa Uganda walisema gari lao lilichomwa moto baada ya kuuawa.

Richard Davies, msimamizi wa kanisa la St Mary's huko Hampstead Norreys, alisema ni viguku kukubali "taarifa hiyo".

"Tunaamka leo tukiwa na huzuni kubwa, kusikia habari mbaya za kifo cha Dave na Celia Barlow," Bw Davies alisema. "Maneno hayawezi kueleza jinsi tulivyopokea habari hii ya kutisha."

Baraza la Parokia ya Hampstead Norreys lilimuelezea Bw Barlow, raia wa Uingereza, kama "mwenyekiti wa kipekee" ambaye alitumikia baraza hilo kwa zaidi ya muongo mmoja.

"Alikuwa nguzo ya jamii, kila mara alitanguliza mahitaji yao," ilisema.

Katika taarifa yake, kampuni ya usafiri ya Belmond, iliyomtaja kama Celia Geyer, ilisema alikuwa "mwanzilishi wa kweli moyoni na kiongozi anayeheshimika sana katika tasnia yetu".

Toby Harris, mjumbe wa baraza la parokia ya kijiji, alisema Bw Barlow "alikuwa mtu wa kweli".

Chanzo: Bbc