Afrika

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

TV

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Maporomoko ya udongo yasababisha vifo vya watu 37 Ethiopia

Watu Kadhaa Wahofiwa Kunaswa Kwenye Maporomoko Ya Udongo Kenya Maporomoko ya udongo yasababisha vifo vya watu 37 Ethiopia

Tue, 1 Oct 2024 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Karibu watu 37 wamepoteza maisha kutokana na mvua kubwa inayoendelea kunyesha kaskazini mwa Ethiopia, ambapo maporomoko ya ardhi na mafuriko yameharibu maeneo mengi ya ukanda huo.

Mihiret Melaku Mkuu wa Ofisi ya kanda ya kuzuia na uratibu wa usalama wa chakula amesema kuwa mifugo isiyopungua 731 imesombwa na maji katika eneo la Wagkhmra katika jimbo la Amhara kaskazini mwa Ethiopia.

Amesema, mafuriko na maporomoko ya udongo yamebomoa nyumba 277 za wakulima. Hadi sasa maporomoko ya udongo yamesababisha vifo vya watu zaidi ya 500 tangu mwezi Julai mwaka huu katika nchi hiyo ya Pembe ya Afrika.

Ripoti nyngine kutoka Ethiopia zinasema kuwa, shule zaidi ya 550 katika jimbo la Tigray kaskazini mwa nchi hiyo zinaendelea kutumika kama kambi za kijeshi. Haya yameelezwa na afisa elimu wajimbo hilo.

Ato Redai G.Ezger Naibu Mkuu wa Kitengo cha Elimu katika jimbo la Tigray ameliambia gazeti la Addis Maleda kuwa shule 552 zingali zinadhibitiwa na makundi yenye silaha; suala linalokwamisha pakubwa ufundishaji wa kawaida na masomo kwa wanafunzi.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live