Afrika

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Maporomoko ya ardhi yaua watu 22 DRC

Maporomoko DRC Amauti.png Maporomoko ya ardhi yaua watu 22 DRC

Wed, 27 Dec 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Maporomoko ya ardhi yaliyosababishwa na mvua mkubwa zilizonyesha hadi jana Jumanne eneo la Kananga, Mji mkuu wa Mkoa wa Kasai-Kati nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo (DRC) yamesababisha vifo vya watu 22.

Shirika la Habari la AFP limesema mvua hizo zilizonyesha jana Jumanne, mbali na vifo hivyo zimesababisha uharibifu mkubwa katikati mwa nchi hiyo na zaidi ya nyumba 15 zimesombwa na maporomoko hayo.

Miongoni mwa matukio ya kusikitisha ni vifo vya mama na watoto wake wanane ambao walikufa katika nyumba moja, wakati baba na watoto wanne wakifariki katika nyumba nyingine.

Katika nchi ya Thailand, AFP imesema mafuriko Kusini mwa Thailand yameua takribani watu sita na kuathiri maelfu ya makazi.

Mafuriko yalianza Desemba 22, 2023 yameathiri zaidi ya nyumba 70,000 katika majimbo ya Satun, Songkhla, Pattani, Yala na Narathiwat, maofisa wa eneo hilo wamesema.

Naibu gavana wa mkoa, Preecha Nualnoi ameiambia AFP kuwa watu sita akiwemo mwanamke mwenye umri wa miaka 89 na mtoto mchanga wamefariki huko Narathiwat.

Pia, ameongeza kuwa mtu mwingine bado hajapatikana kufuatia mafuriko hayo ambayo yamefikia urefu wa mita tatu katika baadhi ya maeneo.

Picha mbalimbali zinaonyesha mitaa iliyokumbwa na mafuriko hayo huku wakazi wakipanda juu ya mapaa.

Idara ya kuzuia na kupunguza maafa ya Thailand imesema kiwango cha maji kimepungua asubuhi ya leo Jumatano Desemba 27,2023.

Taarifa nyingine pia zimesema watu tisa wamekufa baada ya dhoruba kupiga pwani ya mashariki mwa Australia.

Inataarifiwa kuwa dhoruba ya radi na upepo mkali katika siku za hivi karibuni zimekumba majimbo ya Australia ya Victoria na Queensland ambapo imepindua boti, kuzua mafuriko na kuharibu miundombinu ya umeme.

Ofisi ya serikali ya hali ya hewa imeonya kwamba maeneo ya pwani huko Queensland bado yapo katika hatari ya dhoruba, mafuriko, mvua ya mawe, na upepo mkali.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live