Afrika

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Maporomoko ya ardhi yaua watu 14 kwenye mazishi

Maporomoko Ardhi Vifoooo.png Maporomoko ya ardhi yaua watu 14 kwenye mazishi

Mon, 28 Nov 2022 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Watu 14 wamefariki dunia baada ya kutokea maporomoko ya ardhi katika mji wa Yaounde nchini Cameroon.

Kwa mujibu wa gavana wa eneo hilo, Naseri Paul Bea watu hao walikuwa wamehudhuria mazishi jana Jumapili Novemba 27, 2022 jioni.

Mamlaka zinasema kuwa vikosi vya uokoaji bado vilikuwa vinatafuta miili mingine na manusura.

Mashuhuda wamesema kuwa familia kadhaa za waombolezaji zilikuwa zimekusanyika chini ya hema kubwa wakati tukio hilo linatokea baada ya mvua kubwa kunyesha.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live