Kumetokea maporomoko mengine ya ardhi yaliyosababishwa na mvua kubwa mashariki mwa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DR Congo) Watu sita wamethibitishwa kufariki dunia huku zaidi ya wafanyakazi 100 wanahofiwa kukwama ndani ya mgodi ulioporomoka karibu na mji wa Rubaya katika jimbo la Kivu Kaskazini.
Mafuriko na maporomoko ya matope yaliyokumba vijiji viwili kwenye mwambao wa Ziwa Kivu wiki iliyopita yanatajwa kusababisha vifo vya takribani watu 400.
Maelfu ya watu wanaripotiwa kupotea, msemaji wa serikali Patrick Muyaya alitetea jinsi suala hilo linavyoshughulikiwa, huku kukiwa na ukosoaji wa mamlaka kuwa wepesi kujibu suala hilo na kutumia makaburi ya halaiki kuwazika wafu.