Afrika

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Mapinduzi yatokea Sudan, mawaziri kadha wakamatwa

795 BREAKING NEWS1 1 11 660x400 Mapinduzi yatokea Sudan, mawaziri kadha wakamatwa

Mon, 25 Oct 2021 Chanzo: kiswahili.tuko.co.ke

Mapinduzi ya kijeshi yaeripotiwa nchini Sudan kufuatia maandamano ya siku kadha yaliyotaka serikali iliyopo madarakani kuondoka na serikali ya kijeshi kuwekwa.

Waziri Mkuu Abdallah Hamdok aliwekwa mateka nyumbani kwake baada ya kundi la wanajeshi wasiojulikana kuzingira nyumba yake mapema Jumatatu, Oktoba 25.

Jeshi lilitarajiwa kukabidhi mamlaka kwa wananchi mwezi ujaoRipoti pia zinasema, mawasiliano kupitia intaneti yamekatizwa maeneo mengi ya mji mkuu Khartoum

Habari kutoka Al Hadath TV nchini humo zinasema Waziri Mkuu Abdallah Hamdok aliwekwa mateka nyumbani kwake baada ya kundi la wanajeshi wasiojulikana kuzingira nyumba yake mapema Jumatatu, Oktoba 25.

Kwa mujibu wa taarifa hizo mawaziri 4 akiwamo waziri wa Mawasiliano, mwanachama wa halmashauri kuu wametiwa mbaroni.

Shirika hilo limenukuu vyanzo visivyojulikana, na uthibitisho huru haukupatikana mara moja.

Jeshi lilitarajiwa kukabidhi mamlaka kwa wananchi mwezi ujao. Ripoti pia zinasema, mawasiliano kupitia intaneti yamekatizwa maeneo mengi ya mji mkuu Khartoum.

Taarifa zaidi ni baadaye...

Chanzo: kiswahili.tuko.co.ke