Afrika

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Mapinduzi ya Gabon: Rais aomba msaada huku jeshi likichukua madaraka

Ali Bongo Mapinduzi ya Gabon: Rais aomba msaada huku jeshi likichukua madaraka

Wed, 30 Aug 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Rais wa Gabon ametoa wito kwa "marafiki duniani kote" "wapige kelele" kuhusu mapinduzi ya Gabon, katika klipu ambayo imekuwa ikisambazwa kwenye mitandao ya kijamii.

Akiwa ameketi katika kile anachosema ni makazi yake - katika chumba kikubwa kilicho na kuta zilizoezekwa kwa mbao, mazulia ya kifahari na vitabu vya ngozi - Ali Bongo anasema:

"Mwanangu yuko mahali fulani, mke wangu yuko mahali pengine. "Hakuna kinachoendelea. Sijui kinachoendelea."

Anawahimiza tena "marafiki" wake kuzungumza, kabla ya kuwashukuru.

Kampuni ya mawasiliano iliyokuwa ikifanya kazi kwa urais wakati wa uchaguzi imekuwa ikiwasiliana na BBC ili kuthibitisha uhalali wa picha hizo. Imeombwa na ofisi ya Bongo kusambaza video hiyo.

Bongo anaongea kwa Kiingereza. Lugha rasmi ya Gabon - eneo la zamani la Ufaransa, ambalo lilipata uhuru wake mnamo 1960 - ni Kifaransa.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live