Limekuwa tukio la kawaida siku hizi barani Afrika kuwaona askari wachache kwenye TV ya serikali wakitangaza kwamba wamechukua mamlaka ya nchi.
Wakati huu uchaguzi wa udanganyifu ulikuwa kisingizio - Ali Bongo, rais aliyeko madarakani, alikuwa ametangazwa saa chache tu kuwa mshindi wa kura iliyoshutumiwa sana.
Waangalizi wa kimataifa na waandishi wa habari walikuwa wamezuiwa kuufuatilia uchaguzi.
Katika mfumo wa ufadhili ambapo usaidizi unanunuliwa kwa ufanisi, ni vigumu kupima usaidizi wa kweli. Lakini nchini Gabon hakuna shaka kwamba wakiwa madarakani tangu 1967, wengi wwalikuwa wamechoshwa na familia ya Bongo.
Watu waliingia haraka mitaani, wakionekana kuwa na furaha ya kweli.
Hadi sasa hakuna dalili ya kurudi nyuma.
Kwa jamki ya kimataifa, ikiwa ni pamoja na Umoja wa Afrika, hii inaleta hali ya sintofahamu kuhusu ni nini la kufanya.
Ufaransa imeharakishakutoa shutuma zake za kawaida. Ushawishi wake barani Afrika umepungua kwa kiasi kikubwa katika miaka ya hivi karibuni, na mwito wa wa kuunga mkono utawala wa miaka mingi zaidi wa Ali Bongo huenda ukagonga mwamba nchini Gabon.