Kiongozi wa serikali ya Niger Jenerali Abdourahmane Tchiani amemteua waziri wa zamani wa fedha kuwa waziri mkuu mpya kufuatia mapinduzi ya Julai 26.
Ali Mahaman Lamine Zeine anachukua nafasi ya Mahamadou Ouhoumoudou, ambaye alikuwa Ulaya wakati wa mapinduzi.
Bw Zeine, aliyeripotiwa kuwa na umri wa miaka 50, alihudumu kama mkurugenzi wa baraza la mawaziri na waziri wa fedha kuanzia 2001 hadi kupinduliwa kwa aliyekuwa Rais wa zamani Mamadou Tandja na jeshi mnamo 2010.
Uteuzi wake ulitangazwa katika taarifa iliyosomwa kwenye kituo cha televisheni kinachomilikiwa na serikali Télé Sahel Jumatatu usiku na msemaji wa utawala wa kijeshi.
Bw Zeine amefanya kazi katika Benki ya Maendeleo ya Afrika nchini Chad, Ivory Coast na Gabon katika miaka ya hivi karibuni, kulingana na tovuti ya kibinafsi ya ActuNiger.
Jeshi pia siku ya Jumatatu ilimteua Brig Jenerali Amadou Didilli kama mkuu wa Mamlaka ya Juu ya Ujumuishaji wa Amani ya nchi (HACP) na Brig Jenerali Abou Tague Mahamadou kama mkaguzi mkuu wa jeshi na jeshi la kitaifa
Ilimtaja Kanali Ibro Amadou Bachirou mkuu wa watumishi wa kijeshi na Lt Kanali Habibou Assoumane kama kamanda wa walinzi wa rais.