Afrika

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Mapiigano yapamba moto Somaliland, vifo vyaongezeka

Somalia QA 27April2021 1 1140x640 Mapiigano yapamba moto Somaliland, vifo vyaongezeka

Sun, 12 Feb 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Idadi ya vifo kutokana na mapigano katika eneo lenye mamlaka ya ndani Somaliland Somalia imeongezeka na kufikia watu 74.

Taarifa hiyo ni kwa mujibu wa msemaji wa mji unaokabiliwa na mapigano wa Las Anod.

Ghasia zilizuka katika mji huo siku ya Jumatatu, muda mfupi baada ya majimbo matatu katika eneo lililojitenga la Somaliland katika Pembe ya Afrika kutangaza kutaka kuwa sehemu ya Somalia tena.

Majimbo ya Sool, Sanaag na Cayn yanaunda takriban theluthi moja ya majimbo ya mamlaka ya Somaliland.Maeneo hayo yanazozaniwa pande zote mbili Somaliland na mamlaka ya jirani ya Puntland.

Vurugu katika ukanda huo zimedumu kwa majuma kadhaa sasa.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live