Afrika

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Mapigano yazuka katika baadhi ya maeneo ya Sudan

Karthouom Sudan Mapigano yazuka katika baadhi ya maeneo ya Sudan

Mon, 24 Jul 2023 Chanzo: Voa

Mapigano yalizuka katika baadhi ya maeneo ya Sudan katika siku ya 100 ya vita siku ya Jumapili huku majaribio ya upatanishi wa kieneo na kimataifa wa mataifa yenye nguvu yameshindwa kutafuta njia ya kutoka katika mzozo unaozidi kuwa mgumu.

Mapigano hayo yalianza Aprili 15 wakati jeshi na kikosi cha RSF walipoanza kugombea madaraka. Tangu wakati huo zaidi ya watu milioni 3 wamekimbia ikiwa ni pamoja na zaidi ya 700,000 ambao wamekimbilia katika nchi jirani.

Takriban watu 1,136 wameuwawa kwa mujibu wa wizara ya afya ingawa maafisa wanaamini kuwa idadi ni kubwa zaidi.

Si jeshi wala kikosi cha RSF kimeweza kutangaza ushindi huku vikosi vya RSF vikidhibiti mapigano ya ardhini katika mji mkuu Khartoum dhidi ya vikosi vya anga na mizinga ya jeshi.

Miundo mbinu na serikali katika mji mkuu imesambaratika huku mapigano yakienea upande wa magharibi hasa katika smkoa tete wa Darfur na pia kusini ambako kundi la waasi la SPLM-N limejaribu kuchukua eneo.

Chanzo: Voa