Afrika

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

TV

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Mapigano yaripotiwa kwa mara ya kwanza mjini Port Sudan

Watu Tisa Wafariki Katika Ajali Ya Ndege Port Sudan   Jeshi Mapigano yaripotiwa kwa mara ya kwanza mjini Port Sudan

Tue, 19 Sep 2023 Chanzo: Bbc

Mapigano kati ya pande mbili zinazohasimiana za jeshi la Sudan yameenea hadi mji wa Port Sudan kwa mara ya kwanza katika kipindi cha miezi mitano ya vita.

Wanajeshi wa Sudan walifyatuliana risasi na wanachama wa kundi la wanamgambo wa kikabila linalojiita Forces of the Eastern Sudan Parties and Movements Alliance.

Wanajeshi hao walijaribu kuondoa vizuizi vilivyowekwa na kundi hilo siku ya Jumatatu katikati mwa jiji.

Bandari ya Sudan ni mwenyeji wa uwanja wa ndege pekee unaofanya kazi nchini humo.

Mji huo pia ni mahali ambapo baadhi ya maafisa wa serikali na mashirika ya Umoja wa Mataifa wamehamia kutokana na mapigano katika mji mkuu, Khartoum, na kwingineko nchini humo.

Mapigano kati ya jeshi la Sudan na Vikosi hasimu vya Wanajeshi wa Msaada wa Haraka RSF, yamesababisha maelfu ya watu kuuawa tangu ghasia kuzuka katika mji mkuu, Khartoum, mwezi Aprili.

Chanzo: Bbc