Afrika

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

TV

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Mapigano yarindima kaskazini mwa Mali

Jeshi Jeshii Mali Mali.png Mapigano yarindima kaskazini mwa Mali

Wed, 13 Sep 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Hali ya usalama inaendelea kudorora Kaskazini mwa Mali. Waasi wa zamani wa Coordination of Azawad Movements (CMA) na jeshi la Mali wanakabiliana tangu siku ya Jumanne katika eneo la kimkakati la Bourem kaskazini, lililoko kati ya Gao na Kidal. Kila upande unadai ushindi.

Kwa mujibu wa shuhuda zilizokusanywa, huko Bourem, silaha zilianza kusikika mapema Jumanne asubuhi. Watu walisalia majumbani kwao. Moja ya kambi kuu za jeshi la Mali huko kaskazini ililengwa na washambuliaji. Katika taarifa kwa vyombo vya habari, walijitangaza kuwa wanapiganaji wa CMA, muungano wa makundi ya waasi wa zamani. Na kulingana na waasi haoi, walidhibiti ngome za jeshi la serikali kwa muda kabla ya kuondoka eneo hilo na silaha na risasi.

Lakini upande wa jeshi la Mali, taarifa kwa vyombo vya habari inatoa toleo jingine. Hapo awali, wanajeshi wa serikali "walizuia shambulio la mabomu mabomu yaliyokuwa yametegwa katika magari, lililofanywa na magaidi kadhaa" huko Bourem, kulingana na taarifa ya jeshi kwa vyombo vya habari. Jeshi la Mali, FAMA, linadai kutekeleza operesheni ya pili kaskazini mashariki mwa eneo hilo. Jeshi linakiri kuuawa kwa wanajeshi wake kumi na linadai kuwaangamiza washambuliaji 46.

Mvutano unaendelea katika eneo hilo. Kila kambi inaimarisha ngome zake. Na kwa mujibu wa waangalizi, hii ni vita vya kuudhibiti mji wa Kidal unaoshikiliwa na waasi wa zamani ambayo ndiyo kwanza imeanza huko Bourem

Chanzo: www.tanzaniaweb.live