Afrika

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Mapigano yaendelea miji ya Sudan

RSF Ya Sudan Yalaani Vikwazo 'visivyo Vya Haki Vya Marekani Mapigano yaendelea miji ya Sudan

Sun, 5 Nov 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Naibu kamanda wa Kikosi cha Msaada wa Haraka cha Sudan (RSF), Abdel Rahim Hamdan Daglo, amesema kuwa, kundi lake litaendelea kusonga mbele na kuchukua maeneo yanayoshikiliwa na jeshi la nchi hiyo hadi litakapotwa ardhi yote ya Sudan.

Abdel Rahim Daglo ni kaka yake Hamdan Daglo, aliyekuwa Naibu Mkuu wa serikali ya kijeshi ya Sudan na ambaye hivi sasa ni kamanda wa Kikosi cha Msaada wa Haraka, RSF.

Matamshi yake hayo yamekuja baada ya mlolongo wa mafanikio ya RSF ya kuteka maeneo mbalimbali ya Sudan hasa katika eneo Darfur la magharibi mwa nchi hiyo.

Tarehe 30 Oktoba mwaka huu, kikosi cha RSF kilisema kukwa kimechukua udhibiti wa uwanja wa ndege wa Belila na eneo la karibu na hapo lenye utajiri wa mafuta katika Jimbo la Kordofan Magharibi.

Vita baina ya majenerali wa kijeshi Sudan vinaendelea kuisababishia madhara makubwa ya nchi hiyo ikiwemo kutodhibitiwa silaha.

Lakini siku ya Alkhamisi, jeshi la Sudan lilisema kuwa limechukua tena udhibiti wa maeneo hayo mawili.

Pande zinazogombana nchini Sudan zina nia ya kuteka maeneo mengi zaidi kutoka upande wa pili hususan maeneo ya kimkakati licha ya kuweko mazungumzo mapya ya mjini Jeddah Saudi Arabia kwa ajili ya kusuluhisha mzozo uliodumu kwa miezi sita sasa nchini Sudan.

Vita baina ya majenerali wa kijeshi huko Sudan vinaisababishia madhara makubwa nchi hiyo yakiwemo magendo ya silaha ambapo mwishoni mwa mwezi Agosti mwaka huu, kuliripotiwa kuongezeka sana masoko haramu ya silaha nchini Sudan na kuzusha wasiwasi mkubwa miongoni mwa raia hasa katika mji mkuu, Khartoum.

Taarifa zinasema kuwa, bei ya bunduki aina ya AK-47, moja ya silaha za kivita zinazotambulika zaidi duniani, imeporomokka kwa asilimia 50 katika kipindi cha miezi michache iliyopita kwenye soko la biashara haramu katika mji mkuu wa Sudan, Khartoum na hiyo ni hatari kubwa kwa usalama wa Sudan, nje ya Sudan na kwa ukanda mzima wa katikati na mashariki mwa Afrika.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live