Afrika

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

TV

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Mapigano yaendelea Sudan, UN watoa onyo

Mzozo Wa Sudan: RSF Yalaani Mauaji Ya Gavana Wa Darfur Mapigano yaendelea Sudan, UN watoa onyo

Wed, 12 Jul 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Mapigano yanaendelea kati ya jeshi la Sudan chini ya uongozi wa Jenerali Abdul Fattah al-Burhan na vikosi vya msaada wa haraka vya nchi hiyo chini ya uongozi wa Jenerali Hamidti.

Kwa mujibu wa televisheni ya Al Jazeera, milio ya risasi na makombora imeendelea kusikika kati ya pande mbili katika maeneo ya kusini mashariki mwa Khartoum na Omdurman. Jeshi la Sudan linatumia ndege za kivita huku vikosi vya msaada wa haraka vikikabiliana na mashambulio hayo kwa kutumia mifumo ya makombora ya kupambana na mashambulio ya anga.

Kwa upande mwingine, Yusuf Ezzat, mshauri wa kamanda wa Vikosi vya Msaada wa Haraka vya Sudan, ameiambia televisheni ya Al Jazeera kwamba vikosi vyao havishirikiani na mamluki wa kigeni kupambana na wanajeshi waliofanya mapinduzi chini na Jenerali Abdul Fattah al Burhan.

Mshauri huyo wa kamanda wa Vikosi vya Msaada wa Haraka vya Sudan vilevile amesema, kwa upande wao wamepokea vizuri matokeo ya mkutano wa pande nne wa IGAD, wanaunga mkono mpango wa kusitisha mapigano na mipango yote ya nchi za Kiarabu na Afrika za kukomesha mapigano na kutatua mgogoro wa Sudan.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live