Afrika

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Mapigano yaanza tena Mali

Mali Alqaeda Mapigano yaanza tena Mali

Mon, 13 Nov 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Mapigano kati ya jeshi la Mali na wanamgambo wa Tuareg na makundi kadhaa ya waasi yalianza tena jana Jumapili katika eneo la kistratejia la kaskazini mwa nchi hiyo.

Sauti ya mirindimo ya risasi na maroketi zilisika jana kati ya pande hizo karibu na eneo la Kidal kaskazini mwa Mali. Watawala wa kijeshi wa Mali tangu wachukue uongozi wa nchi katika mapinduzi yaliyojiri nchini humo mwaka 2020, wamekuwa wakitoa kipaumbele katika suala la la kuasisi uongozi wa kusimamia maeneo yote; ambapo Kidal inaweza kuwa ngome muhimu ya vita. Ndege za kijeshi za Mali pia zimeonekana zikiruka katika eneo la Kidal jana Jumapili.

Itakumbukwa kuwa msafara mkubwa kijeshi ulipiga kambi huko Anefis tangu mapema mwezi Oktoba mwaka huu. Eneo hilo lipo umbali wa kilomita 110 kusini mwa mji wa Kidal. Wakati huo huo waasi katika mji wa Kidal Ijumaa iliyopita walikata mawasiliano ya simu wakihofia kushambuliwa na jeshi la Mali kufuatia mashambulizi ya anga ya siku kadhaa ya jeshi hilo dhidi yao. Inafaa kuashiria hapa kuwa, watu wasiopungua elfu 25 wanaishi huko katika eneo la jangwa la Kidal; eneo muhimu kwenye barabara ya kuelekea Algeria na ambalo linatambulika kakma eneo la kihistoria la uasi.

Waasi wa Tuareg wa nchini Mali

Wakazi wa eneo hilo wamejiandaa kukabiliana na mapigano tangu waasi wa Tuareg wabebe silaha tena mwezi Agosti mwaka huu. Waasi wa Tuareg waliendesha uasi mwaka 2012 dhidi ya jeshi la Mali ambalo liliibuka na ushindi ambapo waasi walilazimika kusitisha mapigano mwaka 2014 na kufikia mapatano ya amani mwaka 2015.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live