Afrika

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

TV

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Mapigano mapya yaripotiwa baina ya jeshi la Sudan na RSF huko Darfur

RSF Yapinga Mpango Wa Msaada Uliyofikiwa Kati Ya Jeshi La Sudan Na UN Mapigano mapya yaripotiwa baina ya jeshi la Sudan na RSF huko Darfur

Sat, 11 May 2024 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Wimbi jipya la mapigano limeripotiwa kuanza baina ya wanajeshi wa Sudan na wapiganaji wa Vikosi vya Usaidizi wa Haraka RSF katika jimbo la Darfur, magharibi mwa nchi hiyo.

Wanaharakati wa kundi la kiraia la Al-Fasher wameliambia shirika la habari la Anadolu kuwa, mapigano hayo yalianza jana Ijumaa na yanaendelea mpaka sasa.

Habari zaidi zinasema kuwa, watu kadhaa wamejeruhiwa baada ya nyumba zao kushambuliwa kwa maroketi karibu na mji wa Al-Fasher, makao makuu ya jimbo la Darfur Kaskazini.

Inaelezwa kuwa, silaha nzito nzito zimetumika katika wimbi hilo jipya la makabiliano jimboni Darfur. Hata hivyo, mpaka tunamaliza kuandaa taarifa hii, hakuna taarifa iliyokuwa imetolewa na jeshi la Sudan au RSF kuhusiana na vita hivyo.

Wimbi la jipya la mapigano limeanza Sudan katika hali ambayo, Shirika la Kimataifa la Kutetea Haki za Binadamu la Human Rights Watch hivi karibuni lilisema kuwa, mfululizo wa mashambulizi ya vikosi vya wanamgambo vya Sudan katika eneo la Darfur unaongeza uwezekano wa "mauaji ya halaiki".

Chanzo: www.tanzaniaweb.live