Afrika

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Mapigano makali yaua Libya

Ujumbe Wa UN Libya Umeelezea Wasiwasi Wa Watu Kuendelea Kutekwa Mapigano makali yaua Libya

Wed, 16 Aug 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Msemaji huyo wa masuala ya dharura na utoaji misaada nchini Libya amebainisha kuwa mapigano hayo yamesababisha pia vifo vya watu kadhaa, lakini idadi yao bado haijajulikana.

Mapigano hayo yaliyopamba moto jana Ijumaanne, yalianza Ijumaatatu usiku kufuatia kutiwa nguvuni Mahmoud Hamza, kamanda wa Kikosi cha 444 cha askari wa miguu na maafisa wa Idara ya Operesheni na Usalama wa Mahakama inayohusishwa na Kitengo cha uzuiaji hujuma.

Libya imekumbwa na vita na machafuko ya kisiasa tangu mapinduzi ya 2011 ya wananchi, yaliyopelekea kupinduliwa serikali ya kiongozi wa muda mrefu wa nchi hiyo Muammar Gaddafi kwa uingiliaji wa Marekani na baadhi ya nchi za Ulaya na za eneo.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live