Afrika

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Mapigano makali yaripotiwa Kivu Kaskazini, Congo DR

DRC Yadai Rwanda Inafadhili Waasi Wa M23 Mapigano makali yaripotiwa Kivu Kaskazini, Congo DR

Mon, 23 Oct 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Mapigano makali yameendelea kushuhudiwa kati ya waasi wa M23, na wanajeshi wa serikali ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo na makundi mengine ya waasi mwishoni mwa juma hili na kuzua wasiwasi mkubwa Wilayani Masisi jimboni Kivu Kaskazini.

Wakazi wa mji wa Kitshanga wanasema sasa waasi wa M23 wanaudhibiti mji huo.

Baadhi ya wakazi wa eneo hilo wamesema raia kadhaa wa mji huo wamejeruhiwa katika mapigano hayo na kukimbikizwa hospitalini.

Kwa wiki kadhaa sasa, waasi hao wameendelea kupambana na wale wanaojiita Wazalendo, wanaodaiwa kuungwa mkono na wanajeshi wa serikali ya Congo DR.

Msemaji wa kundi linalojiita Wazalendo, ameliambia Shirika la Habari la AFP kuwa mapigano hayo yataendelea, wakati huu ambapo inasemeka yamevuka mpaka na sasa kuingia Wilayani Rutshuru.

Tangu mwezi Oktoba, mji wa Kitshanga umekuwa chini ya doria na vikosi vya majeshi ya Jumuiya ya Afrika Mashariki, ili kuepusha mapigano kati ya makundi hayo mawili.

Serikali ya Kinshasa inakataa kuzungumza na waasi wa M23, ambao inawatambua kuwa "kundi la kigaidi" linaloungwa mkono na Rwanda.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live