Afrika

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

TV

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Mapigano makali yanaendelea huku IDF ikisema njia ya uokoaji ni 'uwanja wa vita'

Mapigano Makali Yanaendelea Huku IDF Ikisema Njia Ya Uokoaji Ni 'uwanja Wa Vita' Mapigano makali yanaendelea huku IDF ikisema njia ya uokoaji ni 'uwanja wa vita'

Wed, 6 Dec 2023 Chanzo: Bbc

Hali inaonekana kuendelea kuwa mbaya kusini mwa Gaza huku wanajeshi wa Israel wakiendelea kuwaonya wakaazi kuhusu operesheni zao zinazolenga Hamas kusini mwa Ukanda huo – hususan katika eneo la Khan Younis ambako Israel inasema inaamini kuwa viongozi wa Hamas wamejificha.

Khan Younis ndicho kilichokuwa kitovu cha mapigano makali hapo jana na ‘’maagizo ya haraka’’ yaliyotolewa kwa raia leo yanaonyesha kwamba taendelea, kulingana na maelezo yaliyotolewa na msemaji wa IDF kwa vyombo vya habari vya Kiarabu, Avichay Adraee.

IDF imesema haitaruhusu raia kutumia barabara ya Salah al-Din - barabara kuu inayovuka urefu wa Gaza inayotumiwa kama njia ya uokoaji kutoka kaskazini mwa Gaza.

Barabara ni "uwanja wa vita" na "hatari sana" kuifikia, Adraee alichapisha kwenye X, ambayo zamani ilikuwa Twitter.

Licha ya tahadhari hizo, vifo vingi vimesababisha hospitali kuu kusini mwa Gaza kuzidiwa - madaktari wanasema wodi zimejaa sana na wagonjwa walimetandazwa kwenye sakafu iliyotapakaa damu.

Kiwango cha mapigano kinamaanisha kuwa watu 600,000 watahamishwa kusini mwa Gaza, kulingana na Umoja wa Mataifa.

Chanzo: Bbc