Afrika

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Mapigano kati ya jeshi na wanamgambo yanaendelea Ethiopia

Mapigano Makali Yaripotiwa Katika Mji Wa Kihistoria Wa Ethiopia Mapigano kati ya jeshi na wanamgambo yanaendelea Ethiopia

Tue, 7 Nov 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Eneo la Ahmara nchini Ethiopia limeripotiwa kuendelea kushuhudia mapigano makali kati ya wanajeshi wa serikali ya shirikisho na wanamgambo wa eneo hilo.

Tume ya Haki za Kibinadamu ya Ethiopia imetangaza habari hiyo na kuongeza kuwa, zaidi ya watu 3,000 wamekimbia makazi yao, nyumba na maduka yameporwa na kuchomwa moto, na mazao kuharibiwa.

Ghasia hizo zilichochewa na uamuzi wa serikali wa mwezi Aprili mwaka huu wa kuvunja na kuunganisha pamoja vikosi vya kikanda. Hatua hiyo ilipingwa na viongozi wa Amhara na wanamgambo wa Fano walikataa kukabidhi silaha zake.

Ghasia huko Amhara ambalo ndilo eneo la karibuni zaidi lililozuka machafuko nchini Ethiopia zimesababisha kutangazwa hali ya hatari mwezi Agosti mwaka huu.

Mwezi huo huo, Umoja wa Afrika uliitaka serikali ya Ethiopia kufanya mazungumzo na wanamgambo katika eneo la Amhara ili kupata suluhu la amani.

Vita nchini Ethiopia vimeathiri uchumi na kuwaacha wengi wakipambana na kupanda kwa gharama ya bidhaa. Jimbo la Amhara la kaskazini mwa Ethiopia

Tarehe pili mwezi huu wa Novemba, Ethiopia iliadhimisha mwaka wa kwanza wa makubaliano yaliyokomesha vita katika eneo la Tigray ambayo yalizuka baada ya serikali ya shirikisho kuchukua hatua zilizopingwa na chama cha TPLF kilichokuwa kinashikilia madaraka ya jimbo hilo la Tigray.

Mwezi Septemba mwaka huu pia, taarifa zilisema kuwa, Wanamgambo wasiopungua 50 wameuawa katika mapigano makali baina yao na jeshi la serikali kuu la Ethiopia kwenye jimbo la Amhara la kaskazini mwa nchi hiyo ya Pembe ya Afrika.

Taarifa ya Jeshi la Ulinzi la Ethiopia (ENDF) ilisema wakati huo kwamba, mapigano hayo yalitokea katika mji wa kihistoria wa Gondar, ulioko katika umbali wa takriban kilomita 700 kaskazini mwa mji mkuu, Addis Ababa.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live