Afrika

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Mapacha Waoa Mke Mmoja, Wampa Mimba

Mapacha 3?fit=600%2C409&ssl=1 Mapacha Waoa Mke Mmoja, Wampa Mimba

Fri, 10 Sep 2021 Chanzo: globalpublishers.co.tz

IMEZOELEKA kuwa mara nyingi mapacha hupenda kuoa/kuolewa na mapacha wenzao lakini mambo yamekuwa tofauti kwa mapacha hawa ambao wamewaacha watu midomo wazi.

Hii ni baada ya ndugu wawili ambao ni mapacha wa kuzaliwa wamemuoa na kuishi naye kinyumba mwanamke mmoja.

Ndugu hao kutoka nchini Rwanda wamemuoa Mary Josaine na kuishi pamoja miaka miwili sasa. Mary anasema alianza mahusiano akiwa binti mdogo na mmoja wa mapacha hao lakini pacha huyo hakumwambia kama ana pacha mwenzake.



Siku moja akiwa kwenye harakati zake alikutana na pacha wa pili ambaye alimfuata na kuzungumza naye akidhani kwamba ndiye mpenzi wake wa siku zote. Kijana yule hakukataa aliyapokea mapenzi ya binti huyo kwa moyo mmoja bila kujiuliza..

Walikwenda faragha na kushiriki naye tendo la ndoa akidhani ndiye barafu wa moyo wake, kumbe pacha wa mpenzi wake, huo ndiyo ulikuwa mwanzo wa kuwa na wapenzi wawili mapacha hao.

Mapenzi yao yaliendelea pasi na binti huyo kujuaana mpaka siku ya siku ambapo binti huyo alikutana nao mapacha wote wawili hali ambayo alishindwa kuwatofautisha. Kila mmoja alionyesha mahaba kwa binti huyo na kusema ameshatembea naye jambo ambalo wao wenyewe liliwashangaza.



Kwa sababu mapacha wanaoshea yai hawatupani waliamua kukubaliana kuendelea kuwa na mahusiano na Mary ambaye naye pia alifurahia uamuzi wao.

Mapacha hao wanasema wamewekeana zamu ya kulala na mke wao huyo, mmoja akilala na mke, mwingine analala chumba cha pili ili kuepusha hisia za mapenzi na kwamba wanaifurahia ndoa hiyo.

Kwa sasa Mary ni mjamzito na anatarajia kupata mtoto, lakini cha kushangaza mtoto huyo hujajulikana atakuwa ni wa yupi kati yao.
Chanzo: globalpublishers.co.tz