Afrika

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Maombi ya Kitaifa: DP Ruto amshauri Uhuru kuhusiana na BBI

48c8bb043be8edb7 Maombi ya Kitaifa: DP Ruto amshauri Uhuru kuhusiana na BBI

Thu, 27 May 2021 Chanzo: kiswahili.tuko.co.ke

Naibu Rais William Ruto alimshauri bosi wake, Rais Uhuru Kenyatta, kuhusu mchakato wa maridhiano (BBI) ambao unaonekana kukwama kufuatia uamuzi wa Mahakama Kuu.

Wakati wa hafla ya maombi ya Kitaifa katika Majengo ya Bunge Alhamisi, Mei 27, Ruto alimtaka Uhuru kumshirikisha pamoja na viongozi wengine ili kujadili mwelekeo wa mswada huo.

Akitoa hotuba yake alinukuu kifungu cha Biblia kilichosomwa na kinara wa ODM Raila Odinga katika hafla kama hiyo mnamo 2018.

"Mengi yalitokea lakini tunaposimama hapa leo, safari za Tanga Tanga zimeisha na reggae pia imesimama. Nadhani lazima tusikilize na tufanye kitu pamoja.

"Waziri Mkuu wa zamani (Raila Odinga) alisema jambo la maana sana (mnamo 2018). Hata alitupa aya ya Bibilia, Isaya 1:18 ambayo inasema 'njooni tujadili pamoja. Labda Mungu anazungumza nasi tena, akituambia tujadili pamoja, " Ruto alisema.

Wakati uo huo aliguzia kuhusu kutawazwa kwa Spika wa Bunge Justin Muturi kuwa msemaji wa Mlima Kenya na vie vile akachambua matukio ya maendeleo yaliyotekelezwa tangu kulipuka kwa Covid-19 Machi 2020.

"Hata katikati ya janga hili, tumekuwa na mambo mazuri; Rais alizindua Bandari ya Lamu, tukapata Jaji Mkuu wa kwanza wa kike (Martha Koome) na pia spika wetu (Muturi) alitawazwa na wazee," akaongeza.

Aidha Rais Uhuru Kenyatta katika hotuba yake alikwepa makabiliano ya moja kwa moja na naibu wake na badala yake kuhusu umuhimu wa kuwepo kwa amani na umoja.

"Mengi ambayo yamesemwa leo yanalenga kutupata tumaini wakati ambapo tunakabiliwa na janga hatari zaidi kuwahi kutokea.

"Tunahitaji kushirikiana na kufanya kazi pamoja na kuwa na matumaini kwamba kweli tunaweza kushinda changamoto hii. Tusisikie wito huo leo na tusahau mafundisho haya kesho," Uhuru alisema.

Chanzo: kiswahili.tuko.co.ke