Afrika

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Maofisa wanne wa IEBC wafukuzwa kazi

Maofisa Pic Data Ibec Maofisa wanne wa IEBC wafukuzwa kazi

Mon, 8 Aug 2022 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Tume ya Haki za Binadamu Kenya (KHRC) kwa kushirikiana na Taasisi ya Inuka Kenya wamefungua shauri chini ya hati ya dharura wakiitaka Tume Huru ya Uchaguzi na Mipaka (IEBC) iweke matokeo ya urais ya kila jimbo mtandaoni.

Kama pingamizi hilo likipita na kushinda litailazimisha IEBC kutengeza fomu namba 34A na 34B ambazo zitakuwa maalumu kwaajili ya kujaza matokeo ya wagombea wa urais wa kila jimbo.

Kwenye uchaguzi wa mwaka 2017, IEBC iliyatoa matokeo ya urais mtandaoni kwa mfumo wa idadi ya kura na asilimia walizopata wagombea bila kuwepo kwa nakala inayoonyesha mgawanyo wa majimbo na kura zao kwa rais kama inavyohitajika na sheria.

KHRC na Inuka Kenya ni taasisi ambazo zinajihusisha na kusimamia haki na utawala bora nchini humo hasa kwa kipindi hiki cha Uchaguzi Mkuu

Chanzo: www.tanzaniaweb.live
Related Articles: