Afrika

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Maneno Imekwisha: DP Ruto apata furaha kuhusu uamuzi wa BBI

Eb34f922943debda Maneno Imekwisha: DP Ruto apata furaha kuhusu uamuzi wa BBI

Fri, 20 Aug 2021 Chanzo: kiswahili.tuko.co.ke

DP Ruto aliwataka waliokuwa wakipigia debe mswada wa BBI kutuliza boli akisema mambo sasa yamekwisha. Amesema kinachoshuhudiwa ni ujumbe wa Wakenya kuwa wakati wa viongozi kushughulikia maslahi yao umefika mwisho.

Amesema sasa wakati umefika viongozi washughulikie masuala ya Wakenya kabla ya kujadili kuhusu nafasi za uongoziNaibu Rais William Ruto ameonekana kufurahia mwelekeo ambao uamuzi wa mahakama ya Rufaa unachukua kusu mswada wa BBI.

Akiongea na wafuasi wake Karen, Ruto aliwataka wapinzani wake kwenye kinyang'anyiro cha kuingia Ikulu kusahau suala la BBI.

Alisema Wakenya sasa hawataki siasa za kubadilisha katiba kwa sababu maslahi yao ni muhimu zaidi.

"The Die is Cast. Hakuna vile wanaweza kurudisha haya maneno nyuma. Tumewaambia imefika kiwanga sasa Wakenya wameamua kabla ya kuongea mambo ya kubadilisha katiba, tutabanga kwanza vile tutabadilisha uchumi," alisema DP Ruto

Ameendelea kupiga vita mswada huo wa marekebisho ya katiba akisema ni njama ya viongozi wachache kujitafutia mamlaka.



"Kabla ya kupanga vile viongozi wataopata vyeo, kwanza tutapanga vile Wakenya milioni mingi ambao hawana kazi watapata kazi. Kabla ya kupanga vile viongozi watagawana mamlaka tutapanga kwanza vile tutawasaidia wakulima, wafanyibishara ili waweze kujimudu," alisema DP.



Amesema wakati umefika viongozi washughulikie maslahi ya Wakenya kwanza badala ya vile watajinufaisha na uongozi.

"Sasa mambo ya mamlaka na vyeo tutaweka pale mwisho kwa AOB," aliongeza DP.

Wandani wa DP Ruto walianza kufurahia uamuzi kuhusu BBI baada ya kuibuka kuwa majaji wa mahakama ya Rufaa walikuwa wakitupilia mbali rufaa.

Seneta mteule Millicent Omanga aliwatania wenzao waliokuwa wakiunga mkono BBI akiwaambia kitumbua kimeingia mchanga.

Hali ilikuwa kama hiyo pia kwa Mbunge wa Kapseret Oscar Sudi aliyeshukuru Mungu akisema amewaokoa Wakenya.

"Mungu wa Yakobo, Mungu wa Isaka, Mungu wa Wakenya ametukomboa leo. Kimeumana!" alisema Sudi.

Chanzo: kiswahili.tuko.co.ke