Afrika

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Man United yavunja benki kwa Haaland

88996 Pic+united Man United yavunja benki kwa Haaland

Wed, 18 Dec 2019 Chanzo: mwananchi.co.tz

London, England. Manchester United imekubali kutoa Pauni76 milioni kumsajili mshambuliaji kinda wa Red Bull Salzburg Erling Braut Haaland mwezi ujao.

Hata hivyo, Haaland atabaki kwa katika klabu yake kwa mkopo hadi mwishoni mwa msimu huu kabla ya kujiunga na Man United.

Kocha wa Man United Ole Gunnar Solskjaer alikuwa akimuwinda kwa nguvu nyota huyo mwenye miaka 19 na ameonekana kushinda vita hiyo kwa kuwa alikuwa akiwindwa na klabu mbalimbali Ulaya.

Kwa muda mrefu Juventus ‘Kibibi Kizee’ cha Turin na Borussia Dortmund zimekuwa zikivizia saini ya Halaand.

Kiwango bora katika mechi za Ligi ya Mabingwa Ulaya kilimuweka sokoni mchezaji huyo wa kimataifa wa Norway.

Solskjaer ambaye pia ni raia wa Norway amevutiwa na Halaand baada yua kufunga mabao 24 katika mechi 22 alizocheaza msimu huu.

“Sitaki kutoa maoni kuhusu tetesi. Inafahamika nini tunataka na nini tunachotaka kufanya,”alisema Solskjaer.

Licha ya kukubali kumpiga bei Salzburg imetoa masharti kwa Man United ikitaka kumtumia Haaland hadi mwishoni mwa msimu huu.

Chanzo: mwananchi.co.tz